Afrika Kusini imeanza jaribio la kwanza la chanjo dhidi ya virusi vya corona barani Afrika.
Chanjo hiyo imefahamishwa kutengenezwa na kituo cha utafiti cha Chuo Kikuu cha Oxford na tayari imeanza kufanyiwa majaribio kwa binadamu nchini Uingereza.
Nchini Afrika Kusini idadi ya watu walioambukiwa virusi hivyo inakaribia kufikisha watu 140,000 huku watu 2,500 wamefariki dunia na bado ni nchi iliyoathiriwa zaidi barani Afrika na janga hilo la Covid-19.
Chanjo inayoitwa ChAdOx1 nCoV-19 inatarajiwa kufanyiwa majaribio kwa watu 2000 waliojitolea nchini humo.
Vipimo vya utafiti vinaendelea nchini Uingereza kwa watu 4,000 huku utafiti mwingine umepangwa kufanyika nchini Brazil kwa watu 5,000.
