Anayejisikia kuomba ruhusa aniombe tu- Rais Magufuli


“Naomba niwaambie tu nawafahamu vizuri Wateule wote niliowapa nafasi, nendeni mkafanye kazi, kuna changamoto nyingi huko Mikoani nendeni mkazitatue” -JPM baada ya kuwaapisha Viongozi mbalimbali leo Ikulu ya Chamwino, Dodoma

“Anayejisikia kuomba ruhusa aniombe tu, nina Viongozi wengine watatu (Ma-DAS) nikitoka hapa nitaenda kuwapa ruhusa, anayetaka kuomba ruhusa, hata Wakuu wa Mikoa anayetaka hata sasa aseme tu nitampa ruhusa, nafahamu wanakoenda huko nako tutashirikiana vizuri” - JPM

“Mfano leo tumemuapisha DC na DED wa Mvomero maana yake waliokuwepo kule wote wameondoka, unawapa nafasi wakasolve matatizo wanaona hapatoshi wanataka wakasolve mahali pengine, ukiwanyima umefanya dhambi mbaya, kwahiyo nimewapa ruhusa” -JPM