Katibu Mkuu wa UPDP achukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais wa Zanzibar


Na ThabitMadai,Zanzibar.



CHAMA cha Muungano wa watu katika Democrasia halisi UPDP, kimeanza rasmi mchakato wa kumtafuta mgombea wa nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitiachama hicho ambapo Katibu Mkuu wa Chama hicho Taifa Hamadi Mohamed Ibrahim amaejitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama hicho.



Zoezi hilo la Uchukuaji wa fomu limefanyika katika ofisi za chama hicho zilizopo Mtoni Kidatu Mjini Unguja  ambapo mgombea huyo alikabidhiwa fomu na Mjumbe wa Halmashauri kuu na Mkurugenzi wa Chaguzi ndani ya UPDP, Barik Ali Omar.



Mara baada ya zoezi hilo Hamadi Mohamed Ibrahim alisema kwamba kilichomsukuma kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo Urais wa Zanzibar ni katiba ya Serikali ya Zanzibar ambapo inaruhusu kila baada ya miaka 5 vyama mbalimbali hushiriki katika chaguziza kuchagua Rais atakae ongoza Zanzibar.



“Ndugu  zangu wanahabarikuwa nmejitokeza kuchukua fomu ya kuomba chama change kinichague niwe mgombea wa nafasi ya Urais haimaanishi Serikali iliyokuwa madarakani haijafanya kitu bali ambapo nmekamilisha malengio ya chama chetu na chama chochote cha Siasa kukamata Dola,”alisema Hamad Mohamed Ibrahim.



Aliongeza kusema Serikali iliyokuwa madarakani imejitahidi kwa kiasi kikubwa kufanya mengi mazuri kwa maslah mapana ya wananchi kwa kuboresha huduma mbalimbali za kijamii.



Alisema endapo chama chake kitampa ridhaa ya kuwa mgombea wa nafasi ya Urais na Wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba wakamamchagua kuwa Rais wa Zanzibar ataendeleza yale yote mazuri ambayo yamefanywa na Serikali iliyopo madarakani.



“UPDP kwa sasa imeshaonesha njia ya kutaka kuongoza Nchi hii ambapo tutaendeleza yale yote mazuri ambapo serikali hii imeanza kuyafanya na kwenda mbali zaidi kutoka katika uchumi wa kati ambao tumeingia hivi sasa na kwenda katika uchumi wa juu zaidi,”alisema Hamadi Mohamed Ibnrahimu.



Hata hivyo alisema kuwa anaahidi kuboresha miondombinu ya barabara pamoja  na kuboesha huduma muhimu za kijamii kama vile maji safi na salama pamoja na huduma za Afya kwa Wanachi.



Katika Maelezo yake Hamadi Mohamed Ibrahim alisema kwamba endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar jambo la kwanza ambalo atahaikisha analiltatua ni changamoto ya udhalilishaji ambayo kwa sasa inaitafuna visiwa hivyo.



“Nawaahidi Wazanzibar endapo chama change kitapata nafasi ya kuongoza visiwa hivi jambo la Udhalilishaji itakuwa ni jambola kwanza kabisa kulifanyia ili kadhia iondoke kabisa ndani ya visiwa hivi” aliseza Hamad Mohamed Ibrahim Mgombea wa Nafasi ya Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama cha UPDP.



Mjumbe wa Halmashauri kuu na Mkurugenzi wa Chaguzi ndani ya UPDP, Barik Ali Omar alisema kwamba kwasasa zoezi lipo wazi kwa wananchama wote ambapo wanahisi wanauwezo wa kugombea nafasi yoyote ndani ya chama hicho wajitokeza kwani wanaendesha zoezi hilo kwa Demokrasia bila ya kumbagua yoyote Yule.