MGOMBEA wa Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Dk. Hussein Ali Mwinyi amewata ka wananchama wa chama cha Mapinduzi CCM visiwani Zanzibar kuvunja makundi na kuungana pamoja katika kukitafutia chama hicho ushindi katika Uchaguzi Mkuu wa Oktaba 2020.
Amesema kwa sasa Chama kimeshaamua kuwa Mgombea ni moja hivyo makundi yote yavunjwe na kuungana pamoja katika kukitafutia Ushindi chama hicho katika Uchaguzi Mkuu.
Kauli hiyo ameitoa leo wakati Sherehe maalumu ya mapokezi yake yaliyofanyika katika viwanjavya Ofisi Kuu Zanzibar ambapo katika Sherehe hizo Maelfu ya Wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wa Chama wamejitokeza katika mapokezi hayo.
Dk Hussein Ali Mwinyi alisema kuwa mchakato wa kumtafuta Mgombea wa Urais wa Zanzibar tayari umeshakamilika hivyo waanchama wote wa chama hicho wanatakiwa kuungana pamoja na kuvunja makundi yote yaliyokuwepo hapo awali na kazi kubwa iliyokuwa mbeleni ni kutafutia ushindi chama hicho.
“Tulikuwa wagombea 31 kwa sasa ameshapatikana mmoja hivyo ni wajibu wetu kuungana pamoja na kuvunja makundi ili chama chetu kishinde kwa kishindo ambapo alisema kuna kila dalili ya kupata ushindi huo” alisema Dk Hussein Mwinyi.
Dk Hussein Mwinyi aliahidi endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar ata yaenzi na kuyatunza na kuyatunza mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964 pamoja na kudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanibar.
“Endapo nitachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar nitahakikisha naenzi mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964, nitadumisha Muungano wetu pamoja na kuhakikisha Amani iliyopo inaendelea” Alisema Dk Hussein Mwinyi Mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CC.
Aidha Dk Hussein Mwinyi alisema kwamba endapo wananchi watampa ridhaa ya kuwa kuongoza Zanzibar atayaendeleza yale pale ambapo ameishia Rais wa Awamu ya saba Dk Ali Mohamed Shein kwa kuendeleza miradi ya Maendeleo.
“Mimi nitaanzia pale ambapo Dk Shein alipoishia lakini katika kuyatekeleza hayo sitokuwa na huruma wala Muhali kwa yoyote ambaye atakuwa Mbaadhirifu wa mali ya Umma,Uzembe pamoja na wale ambao watakao chezea amani na utulivu wa Nchi”alisema Dk Hussein Mwinyi.