Loading...

Jul 1, 2020

EU yawazuia wageni kutoka Marekani ambako hali ya corona inazidi kuwa mbaya

Umoja wa UIaya umefungua mipaka yake leo kwa wageni kutoka nchi 15, lakini sio wa kutoka Marekani ambako afisa mmoja mwandamizi wa afya ameonya kuwa nchi hiyo inaelekea katika mkondo mbaya wakati matukio ya maambukizi ya virusi vya corona yakiongezeka katika majimbo kadhaa.

Umoja wa Ulaya ulikamilisha orodha ya nchi ambazo hali yao ya kiafya inazingatiwa kuwa salama kwa ajili ya kuwakubalia raia wake kuingia katika umoja huo kuanzia leo.

Nchi zilizoondolewa kwenye orodha hiyo ni Urusi na Brazil, pamoja na Marekani ambayo idadi ya kila siku ya vifo imepita 1,000 jana kwa mara ya kwanza tangu Juni 10.

Wasafiri kutoka China, ambako mripuko huo ulianzia mwishoni mwa mwaka jana, wataruhusiwa kwa masharti kuwa China nayo iufungue mlango wake kwa wakaazi wa Umoja wa Ulaya.

Algeria, Rwanda na Tunisia ni nchi tatu za Afrika ambazo raia wake wanaruhusiwa kuingia Ulaya.

KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger