Na Thabit Madai,Zanzibar.
ZOEZI la Uchukuaji wa Fomu ya Mgombea wa Nafasi ya Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia Makini lafunguliwa leo rasmi ambapo Katibu Mkuu wa chama hicho Ameir Hassani Ameir amechukua fomu hiyo na kuahidi endapo atachaguliwa ataboresha sekta ya elimu na Afya visiwani humo.
Ameir ameahidi kuleta mageuzi katika Sekta ya Sayansi na teknologia visiwani Zanzibar endapo chama cha Democrasia makini kitampisha kuwa mgombea wa nafasi ya urais na wazanzibar kumoa ridhaa ya kuongoza visiwa hivyo.
Mara baada ya kupokea fomu hiyo ambapo alikabidhiwa na Katibu wa Organisation ya chama cha Demokrasia Makini John Fulgence Mrere katika ofisi hiyo zilizopo Taveta Mjini Unguja, Ameir alisema kwamba endapoChama chake kinampa nafasi ya kukiwakilisha katika Uchaguzi Mkuu kwa kugombea nafasi ya nafasi ya Urais wa Zanzibar na kupata ridha kwa wananachi anaahidi kuwaletea maendeleo makubwa katika Sekta ya Elimu na Technolojia pamoja na Sekta ya Afya.
Ameir alisema kwamba vipaumbele vyake endapo atachaguliwa kuwa mgombea wa nafasi hiyo na Kupewa ridhaa kwa Wananchi ni kuboresha kwa kasi Sekta ya Elimu nchini ambapo alisema bado haijafikiwa ipasavyo.
“Vipaumbele vyangu ni vingi sana lakini endapo ntachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar naahidi kuboresha Elimu hasa Sayansi na technolojia pamoja na asfya bure kwa Wanzanzibar wote” alisema Ameir Hassan Ameir.
Pia Katibu Mkuu huyo Ameir Hassan Ameir alisema atadumisha Huduma zote muhimu kwa Wananchi kama vile maji safi na salama na kusema kuwa huduma zote zitakuwa ni bure.
Aidha alisema kuwa atahakikisha anakuza Utalii wa Zanzibar wenye tija kwa wananchi wote ambapo atazalisha ajira nyingi kwa vijana na kukuza pato la taifa na pato la mtu mmoja mmoja kupitia Sekta hiyo.
“Endapo ntachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar huduma muhimu kama vile maji safi na salama itakuwa bure lakini ntahakikisha Utalii uliokuwa katika visiwa hivi unawanufaisha wanzanzibar wenyewe kwa kuzalisha ajira nyingi sana” alisema Ameir Hassan Ameir.
Katika Maelezo yake Katibu Mkuu huyo alisema pia atahakiksha Zanzibar inajengeka kimiundombinu ilikuwa mzuri ambapo atashadihisha kujengwa kwa viwanda vikubwa na vidogo kwa lengo la kuongeza uzalishaji pamoja na kuzalisha ajira kwa vijana visiwani humo.
Hata hivyo alisema visiwa vya Zanzibar vina rasimali za kutosha pamoja na fursa mbalimbali hivyo ameahidiendapo atachaguliwa atahakikisha Rasilimali zilizopo zitawanufaisha Wazanzibarna watanzania kwa ujumla.
Nae Katibu wa Organisation ya chama cha Demokrasia Makini John Fulgence Mrere zoezi hilo tayari limeshafunguliwa rasmi tangu Julai 01 hadi Julai 15 ambapo anawakaribisha wanachama wengine wajitokeza kuomba mafasi ya kugombea nafasi mbalimbali kama vile Ubunge, Uwakilishi, Udiwani pamoja na Urais wa Zanzibar na Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa wenye uwezo.
Katibu Fulgence Mrere aliweka wazi bei za fomu kwa Nafasi ya Urais ambao ni shilingi laki tatu, Ubunge na Uwakilishi elfu 50 na Udiwani elfu 10.
Zoezi la Uchukuaji wa Fomu hiyo ya nafasi ya Urais kwa tiketi ya chama hicho limefanyika katika Ukumbi wa Chama hicho zilizopo Taveta Mjini Unguja na kuhudhriwa na Wananchama mbalimbaliwa Chama hicho visiwani Unguja.