MBEYA: Ndugu wafukua maiti iliyozikwa miezi 3



Ndugu wamedai kuwa mara baada ya kutilia mashaka namna kifo cha ndugu yao kilivyotokea, ndiyo maana waliamua kufuatilia hatua zote lengo likiwa ni kuujua ukweli kama ndugu yao alifariki kifo cha kawaida ama aliuawa, kutokana na mazingira ya kifo hicho kuwa ni ya mashaka.

Ndugu hao wameendelea kudai kuwa hata taarifa za kifo cha Tulizo, walizipata kutoka kwa majirani baada ya mume wake Kelvin Mwanjemba kuwa kimya, huku akidai mkewe alifariki akiwa Hospitali ya Chimala, wakati Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo akidai alimpokea mwili wa Tulizo na si mgonjwa.

Mara baada ya mwili huo kufukuliwa ulipelekwa katika Hospitali ya Chimala kwa lengo la kufanyiwa uchunguzi na baada ya madaktari kuchukua vipimo, mwili huo ulizikwa tena kwa mara nyingine usiku wa kuamkia leo Julai 1, 2020.