Ali Irfaan aapishwa kuwa rais mpya wa Guyana


Waziri wa zamani wa makaazi nchini Guyana Irfaan Ali ameapishwa kuwa rais wa taifa hilo dogo la Amerika Kusini na ambalo limeanza kuzalisha mafuta ghafi, baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa mwezi Machi, ambao ulilalamikiwa na kusababisha kura kuhesabiwa upya.

Hisabu ya awali iliyotolewa mwezi Juni ilionesha kuwa Ali kutokea chama cha upinzani cha Maendeleo ya Watu, PPP, alikuwa ameshinda na Marekani ikamtolea wito Rais David Granger kujiuzulu.

Matokeo ya mwisho yamekuja ikiwa ni miezi michache tu tangu kampuni ya mafuta ya Exxon Mobil kuanza uchimbaji mafuta kwenye pwani ya Guyana na kuligeuza taifa hilo masikini lenye wakaazi wasiozidi laki nane kuwa mzalishaji mpya wa mafuta ghafi duniani.

 Kugunduliwa kwa mafuta hayo kumezidisha mpasuko wa kijamii baina ya raia wenye asili ya Kihindi wanaounga mkono chama cha Ali cha PPP na wale wenye asili ya Afrika wanaouunga mkono muungano wa vyama tawala unaoongozwa na Granger. Ali ameahidi kuwaunganisha raia wote.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items