Balozi Seif awataka wananchi kujikinga na corona

 MAKAMU  wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi  amewataka wananchi visiwani humu kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga  na maambukizi ya Virusi hatari vya Corona ambavyo vimeleta fadhaa na taharuki ndani ya jamii na Duniani kwa ujumla.



Balozi Seif amesema Corona ilileta hofu, wasi wasi na simanzi Dunia nzima  hali iliyopelekea baadhi ya Mila na Taratibu za kibadamu kubadilika kama vile  kupeana mikono kuachwa kwa muda ili kuepuka maambukizi ya janga hilo thakili.



Hayo ameyasema leo huko Mahonda Mkoa wa kaskazini Unguja  wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Vifaa vya kinga dhidi ya Virusi vya Corona  kwa matumizi ya Walimu na Wanafunzi wa Shule   12 zilizomo ndani ya Jimbo ambapo hafla hiyo ya kamabidhiano ya vifaa hivyo   imefanyika katika Shule ya Sekondari Kitope.   



Balozi Seif alieleza  kwamba Jamii ibapaswa kuendelea kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona si jambo la hiari bali  ni suala la lazima katika kipindi hichi cha mpito kwa vile maradhi yanayotokana na Virusi hivyo yanaendelea kuitesa Dunia katika baadhi ya Mataifa zikiwemo Nchi za Bara la Afrika.



Hata hivyo Balozi Seif alisema kuwa Serikali ililazimika kupunguza masharti Kumi yaliyoainishwa kupunguza Maambukizi ya Vurusi hivyo baada ya jihitada kubwa iliyochukuliwa na Taifa kwa kushirikiana na Wananchi pamoja na Taasisi za Kitaifa na zile za Kimataifa.



“ Hatua za kunawa Mikono kwa maji ya kutiririka, vitakasa Mikono na uvaaji wa Maski katika maeneo ya msongamano ni vyema ikaendelea kuzingatiwa na kufanywa kama suala la kawaida katika Jamii”. Alisisitiza Balozi Seif.



Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwashukuru na kuwapongeza Wananchi wote Nchini kwa usikivu wao uliopelekea kufuata maelekezo ya Serikali Kuu pamoja na Wataalamu wa Sekta ya Afya na hatimae Taifa kuendelea kubakia salama.

“ Tuna mfano wa Majirani wenzetu wa Mataifa ya Madagaska na Botswana waliofanikiwa kudhibiti kuendea kwa maambukizi ya Virusi vya Corona na kuamua kulegea vikwazo kwa hatua kubwa ambayo sasa inawagharimu kutokana na kasi kubwa ya kurejea upya kwa Maambukizi ya Virusi hivyo”. Alitanabahisha Balozi Seif.

Alisisitiza umuhimu wa Wanafunzi na Walimu Maskulini kuendelea kuvitumia Vifaa vya Kinga kutokana na maeneo yao makubwa kuendelea kuwa na msongamano mkubwa wa Watu.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaomba Wananchi hao kwa vile yeye anapumzika Utumishi wa Jimbo washirikiane na Viongozi wao wa Mahonda Mpya iliyokuja baada ya marekebisho ya Mipaka iliyofanywa hivi karibuni na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC)

Akitoa shukrani kwa niaba ya Walimu Wakuu wa Skuli zilizokabidhiwa Vifaa hivyo vya Kujikinga ya Virusi vya Corona Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari Kitope Mwalimu Simai Haji Hamad alisema wao kama wasimamizi wa Wanafunzi wa Skuli hizo wako tayari kuona vifaa walivyokabidhiwa vinatumika kwa lengo husika.



Vifaa vilivyotolewa na Balozi Seif Ali Iddi vyenye thamani ya Shilingi Milioni 44,000,000/- ni pamoja na Sabuni, Ndoo, Vitakasa Mikono pamoja na vifaa vya kuhifadhia Pua na mdomo { Maski}.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia