Botswana yarejesha agizo la kusalia majumbani


Botswana imerejesha tena marufuku ya kutoka nje kuanzia saa sita usiku kwa muda wa wiki mbili katika mji mkuu wa Gaborone. hatua hiyo imechukuliwa ili kudhibiti wimbi jipya la maambukizi ya virusi vya corona lililozuka.

Wanaofanya kazi muhimu tu ndiyo wataruhusiwa kutoka majumbani mwao, na watu wengine wataruhusiwa kutoka kwenda kununua chakula na mahitaji mengine muhimu.

Mikusanyiko yote ya watu imepigwa marufuku, na mikahawa, shule na hoteli zimeamriwa kufungwa. Botswana iliondoa agizo la karantini mnamo Juni 15, na maeneo ya biashara pamoja na shule zilifunguliwa tena.

Lakini taifa hilo limeanza kushuhudia ongezeko jipya la maambukizi ya corona, hasa katika shule za mjini Gaborone.