https://monetag.com/?ref_id=TTIb Kiongozi wa kidini akamatwa Korea Kusini kwa kuzuia mapambano ya corona | Muungwana BLOG

Kiongozi wa kidini akamatwa Korea Kusini kwa kuzuia mapambano ya corona


Kiongozi wa kanisa la Shincheonji Church of Jesus nchini Korea Kusini Lee Man hee amekamatwa kwa madai ya kuzuia juhudi za serikali za kupambana na janga la virusi vya corona.

Lee anadaiwa kutoa rikodi na orodha za uongo kuhusiana na mikusanyiko ya ibada kwa wahudumu wa afya.

Msemaji wa mahakama ya wilaya ya Suwon ameliambia shirika la habari la AFP kwamba kiongozi huyo alipelekwa mahabusu mapema leo baada ya korti kutoa waranti wa kukamatwa kwake majira ya saa saba za usiku .

Zaidi ya nusu ya waumini wa kanisa hilo ambalo mara nyingi hukosolewa kuwa na imani potofu walikuwa miongoni mwa waathirika wa virusi vya corona nchini humo kati ya mwezi Februari na Machi, wakati taifa hilo lilipokuwa likipambana na mripuko mbaya kabisa wa corona ulimwenguni.

Kulingana na kituo cha kudhibiti magonjwa nchini humo, hadi Julai waumini 5,200 wa madhehebu hayo walikuwa wameathirika na kufanya kiwango cha maambukizi kufikia asilimia 38.