Mbarawa: Nimefarahi sana kuwa Waziri wa Maji wa nchi hii


Waziri wa Maji nchini Makame Mbarawa ametoa wito kwa watumishi wa Mamalaka ya Maji Safi na Usafi Wa Mazingira Mjini Mtwara (MTUWASA)  kubadilisha mitazamo juu ya utendaji kazi ili kufikia malengo ya Serikali juu ya kutatua changamoto za maji kwa wananchi.

Ameyazungumza hayo wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya maji iliyozinduliwa katika ukumbi wa Benki Kuu (BOT) Mkoani Mtwara.

Mbarawa amesema watendaji wengi katika idara za maji nchini wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea na kupelekea kuyumbisha upatikanaji wa huduma  muhimu ya maji na kuendelea kuwa changamoto kwa wananchi.

Ametumia nafasi hiyo kuitaka bodi mpya kujitafari na kuweka mikakati thabidi itayoongeza nguvu ya utendaji na uzalishaji wa maji Mjini Mtwara na kuchangia kupunguza kero hiyo.

Awali akisoma risala ya bodi ya MTUWASA Mkurugenzi wa Mamalaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mjini Mtwara (MTUWASA)  Mhandisi Rejea Ng’ondya ameeleza kuwa hali ya uzalishaji wa maji hadi kufikia Julai 31, 2020 ni asilimia 70 na uhitaji wa maji ni tani Milion 18 kwa siku.

Aidha amesema hadi sasa mamlaka inauwezo wa kuzalisha tani Milion 9.5 hadi Milion 10. 5 kwa siku.

Waziri amesema kuwa amefurahishwa kuwekwa kwenye wizara hiyo kwani kuna umuhimu mkubwa kwa wananchi kufahamu juu matatizo na upatikanaji wa maji hapa nchini.

Aidha Waizri Mbarawa ametoa wito kwa Mkurugenzi wa Mtuwasa kujitafakari juu ya utendaji kazi wake huku akissistiza na ni vyema kuiacha alama ndani ya miezi mitatu umeweka alama gani.;”Mkurugenzi lazima ujitafakari juu ya utendaji kazi wako baada ya miezi mitatu inatakiwa uache alama juu utendaji wako”

Mwenyekiti wa Bodi aliyemaliza muda wake Dr.Shomari Shamte ameongeza kuwa Mamlaka ya maji safi na mazingira Mjini Mtwara( MTUWASA) imefanikiwa kulipa deni la zaidi Milioni 400 kwa  Shirika la umeme nchini  Tanzania (TANESCO)

Lakini pia Waziri Mbarawa amesisitiza kuwa kwa sasa mipango iliyowekwa na Wizarar hiyo ya Maji itahakikisha inasghulikia na kutatua  matatzo ya wananchi juu ya kutokapakana kwa maji Mkoani Mtwara.

Post a Comment

0 Comments