Na Faruku Ngonyani, Mtwara.
Naibu Waziri wa kilimo Omary Mgumba amelitaka Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogovidogo Tanzania (SIDO) kuongeza kasi katika kushughulikia changamoto zinazowakabili wabanguaji wadogowadogo wa Korosho nchini.
Wito huo umetolewa leo katika maonesho ya wakulima Nanenane Kanda ya Kusini Mashariki yanayofanyika katika viwanja Ngongo Manispaa ya Lindi, ambapo amesema wakifanya hivyo itakuwa wamewasaidia wakulima kuongeza thamani katika mazao yao.
Mh.Mgumba ni mgeni rasmi katika maazimisho ya siku ya korosho ambayo yameandaliwa na Bodi ya Korosho Tanzania, ambayo yanafanyika katika maonesho hayo.
