Corona imerudisha maendeleo ya dunia nyuma miaka zaidi ya 20


Ripoti ya utafiti wa wakfu wa Bill & Melinda Gates imebainisha kuwa kusambaa vya virusi vya corona kote duniani kumerudisha nyuma maendeleo ya dunia kwa miaka zaidi ya 20.

Kulingana na utafiti huo, mamilioni ya watu duniani wamezidi kuishi zaidi katika maisha yanayotofautiana, magonjwa na umasikini.

Wakfu huo wa Bill & Melinda Gates unasema kuwa hali hiyo inaathiri malengo mengi ya Umoja wa mataifa yanayolenga kuleta maendeleo duniani.

Akizungumza na BBC, Bill Gates alisema kuwa chanjo ya Covid-19 iliyotengenezwa na kufikia kiwango stahiki huenda ikapatikana mwaka ujao wa 2021.




Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items