Guterres kuyataka mataifa ya dunia kusitisha mapigano hadi Disemba


Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres atatumia hotuba yake ya kila mwaka kwa viongozi wa dunia wiki ijayo kusukuma ajenda yake ya kusitisha mapigano duniani hadi mwishoni mwa mwaka 2020 ili nchi ziweze kupambana na janga la virusi vya corona.

 Guterres hata hivyo alisema fursa zitakuwa zimepotea kwasababu viongozi wa mataifa hawatakuwapo binafsi mjini New York kwa ajili ya mkutano huo. 

Guterres amesema usitishaji wa mapigano duniani utaimarisha juhudi za kupambana na COVID-19 na kusaidia kurejea katika hali ya kawaida kwa njia iliyoratibiwa vizuri na endelevu. 

Hapo kabla alitoa wito wa kusitishwa mapigano tarehe 23 mwezi Machi, lakini uungwaji mkono rasmi kutoka kwa wanachama 15 wa Barza la Usalama la Umoja wa Mataifa ulichukua zaidi ya miezi mitatu, kwasababu ya mkwamo kati ya China na Marekani. 

Marekani haikutaka azimio hilo lizungumzie kuhusu shirika la afya Ulimwenguni WHO, wakati China ilitaka hivyo.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items