Kiongozi mpya wa Baraza la Umoja wa Mataifa

 

Katika hafla hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya UN, Bozkır alichukua madaraka kutoka kwa Rais wa 74 wa Baraza la Umoja wa Mataifa Tijjani Muhammad-Band.

Katika hotuba yake katika Mkutano Mkuu wa UN, Bozkır amesema kuwa janga la Corona limebadilisha mipango ya Mkutano Mkuu wa 75 wa UN, na kuongeza kuwa,

"Barakoa zetu leo zinatukumbusha tishio kubwa sana ambalo tunakabiliwa nalo, maisha tuliyopoteza, shida tunazopaswa kukabiliana nazo na kwamba sisi sote tunapambana na kitu kimoja".

Akisema kwamba janga hilo limetumiwa na wakosoaji wa mfumo wa pande nyingi kuhalalisha hatua za upande mmoja na kudhoofisha mifumo ya kimataifa, Bozkır amebainisha kuwa katika kipindi hiki, mifumo na mashirika ya kimataifa bado yanahojiwa na kwamba ukosoaji huu ulikuwa wa msingi, lakini kulifikiwa hitimisho lisilo sawa.

Bozkır, ambaye ametoa ujumbe wa mshikamano, ushirikiano na kuimarisha imani kwa taasisi za kimataifa dhidi ya janga hilo, ambalo ni mgogoro wa ulimwengu, amesema,

“Hakuna nchi inayoweza kushinda janga hili peke yake. 'Social distancing' haitasaidia katika kiwango cha kimataifa. Hatua za upande mmoja huimarisha tu janga hilo na kutuweka mbali na lengo letu la msingi. Katika nyakati kama hizi za shida, ni jukumu letu la msingi kuimarisha imani katika ushirikiano wa kimataifa na taasisi za kimataifa za UN "

Post a Comment

0 Comments