Msajili: Muungano wa vyama unapaswa kuwasilishwa kwa msajili miezi 3 kabla ya uchaguzi


Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini imesisitiza kuwa vyama vinapaswa kuheshimu Sheria vinapoingia katika ushirikiano wa aina yoyote ama miungano kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu

Kwa mujibu wa Sheria na taratibu vyama vinapotaka kuungana vinapaswa kuwasilisha taarifa ya ushirikiano au muungano huo kwa Msajili wa Vyama miezi 3 kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi

Aidha, Vyama vinakumbushwa kuwa ni wajibu wa Msajili wa Vyama vya Siasa kuchukua hatua za kisheria pale Chama kinapokiuka Sheria na Msajili hatasita kuchukua hatua stahiki za kisheria pale itakapothibitika chama cha Siasa kimekiuka Sheria hizo.


Post a Comment

0 Comments