Umoja wa Mataifa wasema ukosefu wa chakula umerudi tena Yemen

 


Mkuu wa misaada ya kiutu katika Umoja wa Mataifa ameonya kwamba uhaba wa chakula umerudi tena katika nchi iliyozongwa na machafuko ya Yemen. 

Mark Lowcock amezitaja Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu pamoja na Kuwait kama nchi ambazo hazijatoa msaada wowote katika kiasi cha dola bilioni 3.4 zinazohitajika mwaka huu. 

Lowcock amesema Umoja wa Mataifa ulilimaliza tatizo hilo nchini Yemen mwaka jana kwa kuwa wafadhili walitoa haraka michango iliyofikia asilimia 90 ya kiwango jumla kilichoombwa. 

Mkuu huyo amesema maisha ya mamilioni ya watu yaliokolewa kwasababu misaada iliongezwa. 

Ila kwa sasa anadai kwamba ni asilimia 30 tu ya kiasi cha pesa kilichoitishwa ambacho kimetolewa na kwamba Wayemen milioni tisa wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa chakula, maji na matibabu.


Post a Comment

0 Comments