Watano wafariki dunia katika ajali ya basi


  Na Hamisi Nasri,Masasi.

   WATU Tanao (5) wamefariki dunia na wengine sita (6) kujeruhiwa baada ya gari la abiria basi aina ya TATA kuacha njia na kuligonga Gari aina ya Isuzu Jane .

  Ajali hiyo imetokea jana majirà ya saa  7 mchana katika kijiji cha Msanga kata ya Mitesa mpakani mwa wilaya ya Masasi na wilaya ya Newala , mkoani Mtwara. 

Majeruhi hao sita na miili ya watu waliofariki, walipelekwa katika Hospitali ya Wilaya Newala. 

  Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, Mark Njera amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwatakà madereva wa vyombo vya moto kuwa waangalifu barabarani kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani zinavyowaelekeza.

  Kamanda Njera alisema kuwa basi hilo la abiria lilikuwa likitokea wilayani Masasi kuelekea wilayani Newala hadi Tandahimba.

  Alisema lilipofika maeneo ya kijiji cha Msanga kata ya Msanga ndipo lilopokutana na Gari aina ya Isuzu Jane yenye namba za usajili T-311 AER. ambalo lilikuwa likitokea wilayani Newala kuelekea kijiji cha Mchauru kata ya Mchauru wlayani Masasi mkoani Mtwara.

  Kamanda Njera alisema Magari hayo yaligongana uso kwa uso jambo ambalo ilipelekea watu tano kufariki dunia na watu wengine sita kujeruhiwa.

  Alisema miili ya marehemu hao na majeruhi walikimbizwa katika hospitali ya wilaya Newala ambapo maiti zimehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti.

"Tunaendelea kuwasihi madereva wa vyombo vya moto kuzingatia sheria zote za usalama barabarani ili kunusuru maisha watu wasio na hatia kama kila dereva akifuata sheria kikamilifu ajali zitapungua''alisema Kamanda Njera

    Alisema wananchi wanatakiwa kwenda hospitali ya wilaya Newala kwa ajili ya kwenda kutambua miili ya marehemu hao ili kuwapata ndugu na jamaa wa marehemu.

  Baadhi ya baadhi mashushuhuda wa ajali hiyo walisema kuwa changamoto ya ubovu wa barabara hiyo ndio chanzo cha kuwepo kwa matukio ya ajali hususan eneo hilo.

Post a Comment

0 Comments