Umoja wa Mataifa (UN) umeripoti kuwa watu milioni 1 wameathiriwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa za msimu nchini Ethiopia na takriban watu elfu 300 wameyahama makazi yao.
Katika taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Uratibu wa Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, imeelezwa kuwa mvua kubwa na ya muda mrefu katika maeneo tofauti ya nchi hiyo imesababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi, na kuwafanya watu takriban elfu 300 kuhama makazi yao tangu mwezi Juni.
Katika taarifa hiyo, ambayo imesema kwamba mvua hiyo iliathiri watu milioni 1 katika majimbo ya Afar, Oromiya, Gambella, Kusini, Somalia na Amhara na kuwaacha wamekata tamaa, imeonywa kuwa mafuriko hayo pia yameharibu taasisi za afya na kumekuwa na uhaba wa dawa.
Taarifa hiyo imeendelea kwa kusema kuwa kwa sababu ya kuzorota kwa hali ya usafi, hatari ya kuongezeka kwa maambukizi ya corona na ugonjwa wa kipindupindu na magonjwa yanayosababishwa na maji imeongezeka; Imeelezwa kuwa dola milioni 40 zinahitajika kwa ajili ya misaada katika nyanja tofauti , haswa nyumba, chakula na afya.
