Loading...

Sep 19, 2020

Yanga yakamata usukani wa VPL

 


Timu ya soka ya Yanga sc imefanikiwa kupata ushindi wao wapili mfululizo katika ligi kuu ya soka Tanzania bara baada ya kuifunga timu ya Kagera sugar kwa bao 1-0 katika mchezo uliopigwa dimba la kaitaba mjini bukoba.


Katika mchezo huo bao la Yanga limefungwa na kiungo mkabaji raia wa Kongo Mukoko Tonombe katika Dakika ya 71 ya mchezo baada ya kuunganisha pasi Kutoka kwa winga Tuisila Kisinda.


Nahodha wa Yanga Deus kaseke amesema wamecheza na timu nzuri na timu hiyo ilikosa Bahati huku wao wakitumia nafasi waliyopata.


Ushindi huo ni wa sita mfululizo kwa Yanga dhidi ya Kagera katika Uwanja wa Kaitaba kama ambavyo reodi zinavyoonyesha tangu msimu wa 2015/16.


Yanga sc sasa inaongoza ligi baada ya kufikisha jumla ya pointi 7 baada ya kushuka dimbani mara 3 huku wakitarajia kucheza wiki ijayo dhidi ya Mtibwa sugar katika dimba Jamhuri Mjini Morogoro.


Katika mchezo mwingine uliopigwa mapema leo huko mkoani Rukwa, Tanzania Prisons imepata ushindi wake wa kwanza wa VPL kwa kuinyuka Namungo bao 1-0 .

KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger