Yoshihide Suga aidhinishwa kuwa Waziri Mkuu mpya wa Japan



 Bunge la Japan leo limethibitisha kiongozi wa chama tawala cha Liberal Democratic Party LDP Yoshihide Suga ndiye Waziri Mkuu wa 99 wa nchi hiyo. 

Waziri Mkuu huyo mpya anakabiliwa na changamoto ya moja kwa moja ya kupambana na janga la virusi vya corona Japan na uchumi uliodorora pakubwa. 

Suga ambaye alipata ushindi mkubwa wa uongozi wa LDP hapo juzi, ameidhinishwa na mabunge yote yanayoongozwa na chama cha LDP na chama kidogo katika serikali ya muungano cha Komeito. 

Suga mwenye umri wa miaka 71 ambaye ameahidi kuendeleza sera za mtangulizi wake Shinzo Abe, anatarajiwa kuunda baraza lake la mawaziri baadae leo.

 Anatazamiwa pia kuwateuwa mawaziri waliokuwa katika baraza lililopita kama Waziri wa fedha Taro Aso na Waziri wa mambo ya kigeni Toshimitsu Motegi.

Post a Comment

0 Comments