Ditopile aeleza mafanikio ya Serikali ya Dk. Magufuli kwenye sekta ya elimu

Mgombea Ubunge Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma CCM, Mariam Ditopile akiwa kwenye mahafali ya kidato cha nne Sekondari ya Majereko wilayani Chamwino, amesema ndani ya kipindi cha miaka mitano cha Rais Dk John Magufuli zaidi ya Sh Trilioni 1.1 zimetumika kwa ajili ya elimu bila malipo Ikiwa ni sera ya Dk Magufuli kuhakikisha kila mtanzania anapata elimu bila kulipa ada kuanzia Shule ya Msingi hadi Kidato cha Nne.

" Suala la elimu bure ni moja kati ya ahadi za Dk Magufuli kwetu alipokua anaomba ridhaa kwa mara ya kwanza na hakika amefanikiwa sana, watu wengi wanadhani ni elimu bure la hasha ni elimu bila wazazi kulipa ada kwa sababu Rais Magufuli alisema ada italipwa na serikali yake, zipo Nchi kubwa zenye rasilimali kushinda sisi lakini wanashangaa sisi tumewezaje, niwaombe muungeni mkono Rais Magufuli na serikali yake katika hili wametushika mkono wengi sana.

Sekta ya elimu imepiga kasi sana, Shule za Sekondari zimeongezeka kutoka 4708 mwaka 2015 hadi 5330 mwaka huu, shule kongwe zimeboreshwa na leo tunaona matokeo ya mwisho ya kidato cha sita shule za serikali saba zimeingia 10 bora, lakini madawati yameongezeka kutoka Milioni 3 hadi Milioni 8.9 huku vyuo zaidi ya 70 vya ufundi vikijengwa Nchi nzima na sisi Dodoma tumepata pia," Amesema Ditopile.


Katika mahafali hayo Ditopile ameahidi kushirikiana na wananchi kuweza kukamilisha ujenzi wa jengo la mahabara pamoja na kuahidi kuwaletea Kompyuta na Mashine ya Kuchapa ili ziweze kuwasiliana katika kuandaa mitihani na taarifa mbalimbali za shule hiyo.

 

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia