Helikopta ya kijeshi ya Mi8 inayomilikiwa na Urusi iliingia kimakosa kwenye anga ya Hokkaido kaskazini mwa Japan.
Kulingana na taarifa ya Wizara ya Ulinzi ya Japan, helikopta ya jeshi ya Urusi Mi8 iliingia kwenye anga ya Japan mnamo saa 12.25 jioni saa za Japan kwenye uwanja wa Shiretoko mashariki mwa Hokkaido.
Helikopta hiyo, ambayo iliingia kwenye anga ya Japan kimakosa iliondoka bila kufanya vurugu wala fujo baada ya kuonywa na ndege za vita za Kikosi cha Kulinda Anga cha Japan (ASDF).
Baadaye tukio hilo lilitaarifiwa kwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi, mjini Moscow.
