Kiongozi wa upinzani Belarus aomba msaada wa Ujerumani


Kiongozi wa upinzani wa Belarus anayeishi uhamishoni, Svetlana Tikhanovskaya ametoa wito kwa jumuia ya kimataifa ikiwemo Ujerumani kuisaidia nchi yake inayokumbwa na mzozo wa kisiasa. Akizungumza na DW, Tikhanovskaya amesema msaada wa Ujerumani ni muhimu zaidi kwani ni moja ya nchi zenye nguvu kubwa duniani. 

Matamshi hayo ameyatoa jana usiku kabla ya mkutano wake na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel utakaofanyika leo mjini Berlin. 

Msemaji wa Merkel, Ulrike Demmer amethibitisha kuwa mzozo wa baada ya uchaguzi nchini Belarus utakuwa ajenda kuu katika mkutano huo. 

Kiongozi huyo wa upinzani pia anatarajiwa kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Heiko Maas kesho Jumatano. 

Tikhanovskaya ambaye hivi karibuni alikutana na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron anajaribu kutafuta msaada wa kimataifa ili kuongeza shinikizo kwa rais wa muda mrefu wa Belarus, Alexander Lukashenko.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia