Koka apania kuwajengea zahanati wananchi wa kata ya Korogwe

 


NA VICTOR MASANGU, KIBAHA


Mgombea Ubunge wa jimbo la Kibaha mjini Slvestry Koka ameahidi kulivalia njuga suala la changamoto inayowakabili wananachi hususan wakinamama wajawazito kwa kuhakikisha anapambana kwa kushirikiana na serikali ili kujenga kituo cha afya pamoja na ujenzi wa kituo cha polisi ili kuwaondolea adha wananchi ya kutembea umbari mrefu kwenda kufuata huduma.


Koka aliyasema  hayo wakati  akizungumza na wananchi wa kata ya kongowe katika mkutano wake wa kampeni kwa ajili ya kujinadi sera zake pamoja na kuelezea mikakati yake ambayo ataifanya ya kuwaletea wananchi maendeleo endapo i atachaguliwa tena katika kipindi kikingine cha miaka mitano katika uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika octoba 28 mwaka huu.


Alisema kwamba anatambua kuwa kuna changamoto kwa wananachi wa kata ya kongowe juu ya suala la upatikanaji wa huduma ya afya pamoja na kituo cha polisi hivyo atahakikisha kwamba anashirikiana na serikali katika kuanzisha mradi wa ujenzi katika maeneo hayo ili kuweza kuwasaidia wananchi kuondokana na usumbufu ambao wamekuwa wakiupata.


“Naombeni katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu msifanya makosa kitu kikubwa ni kuendelea kuniamini mimi ili niweze kuendelea kutatua changamoto mbali mbali amabzo zinawakabili wananchi na kitu ambacho ninaweza kusema nitakisimamia kwa nguvu zangu zote ni kuanzisha mpango wa ujenzi wa zahanati, kituo cha afya pmoja na ujenzi wa kituo cha polisi,”alisema Koka.


Alifafanua kuwa endapo ujenzi wa kituo cha afya utakapokamilika utakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa kata ya kongowe pamoja na maeneio mengine ya jiraji kuweza kupata huduma ya matibabu kwa ukaribu na kuondokana kabisa na changamoto ya kwenda kufuata huduma hiyo katika maeneo ya mbali.


Pia aliongeza kuwa wananachi wa kata ya kongowe baadhi yao wamekuwa wakipata usumbufu mkubwa pindi masuala ya uharifu yanapojitokeza hivyo ataweka mipango madhubuti kwa kushirikiana na wananchi kuweza kupata ujenzi wa kituo cha polisi ili kusaidia kutoa huduma ya ulinzi pamoja na mambo mengine ya kiusalama.


Katika hatua nyingine Mgombea huyo alisema kwamba lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba anaweka mikakati mizuri amabyo itaweza kuwasaidia wananchi kuondokana na wimbi la umasikini kwa kuhakikisha kuwa anaviwezesha vikundi mbali mbali vya ujasiriamali ili viweze kufikia malengo ambayo vimejiwekea katika kukuza uchumi wao.


Kwa upande wake Mgombea udiwani wa kata ya Kongowe kupitia tiketi ya CCM  Hamisi Shomari alisema  kwamba endapo atachaguliwa katika uchaguzi mkuu atahakikisha kwamba anashirikiana bega kwa bega Mbunge katika kutatua changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi katika  huduma mbali mbali za kijamii ikiwemo suala la huduma ya maji safu na salama pamoja na  elimu.


Naye Mke wa mgombea huyo  Selina Koka  hakusita  kupanda jukwani  na kupiga magoti  kwa ajili ya kumwombea kura mumeo  na kuwahimiza wananchi  wa kata ya kongowe na waweze kumchagua kwa kishindo ili aweze kutatua changamoto zao na  kuwaletea chachu ya  maendeleo.

Post a Comment

0 Comments