Libya kuanzisha tena safari za ndege za Tripoli na Benghazi


Safari hizo za ndege zilikuwa zimesitishwa kwa kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja kutokana na mashambulizi ya wanamgambo wa kundi la silaha linaloongwa na Khalifa Hafter mashariki mwa Libya.

Kulingana na taarifa za kituo cha televisheni cha al-Ahrar nchini Libya, iliarifiwa kuwa baada ya usitishaji wa safari kwa zaidi ya mwaka, ndege moja ilianza msafara wa kuruka kutoka uwanja wa kimataifa wa Mitiga mjini Tripoli, na kutua kwenye uwanja wa kimataifa wa Benina mjini Benghazi.

Mkuu wa shirika la ndege la Afriqiyah Airways nchini Libya Milad al-Hajrasi, alitoa maelezo kwenye televisheni ya Panorama na kutangaza kuwa safari za ndege za kibiashara zitaanzishwa rasmi tarehe 23 Oktoba kati ya uwanja wa kimataifa wa Mitiga, na uwanja wa kimataifa wa Benina.

Hajrasi aliongezea kusema kuwa shughuli za matengenezo ya viwanja hivyo viwili vya ndege pia imekamilishwa.

Uwanja wa kimataifa wa Benina  ulioko Benghazi ambao ni mji wa pili kwa ukubwa nchini Libya, ulilazimika kufungwa mwezi Aprili mwaka 2019 kutokana na mashambulizi ya kundi la Hafter.

Post a Comment

0 Comments