Mkenge azungumzia mikopo binafsi ya halmashauri


 

Na Omary Mngindo, Yombo.

MGOMBEA Ubunge Jimbo la Bagamoyo Mkoa wa Pwani Muharami Mkenge, amesema kuwa akichaguliwa kushika nafasi hiyo katika mambo atayofuatilia ni pamoja na kukaa na Halmashauri kuangali mikopo ya watu binafsi.

Sanjali na hilo pia mikopo kwa akina baba wenye umri wa kati wenye uwezo wa kumiliki biashara zitazosaidia kuajiri wengine, tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo kuna mikopo ya Vijana, Wanawake na watu wenye Ulemavu tu.

Mkenge alisema kuwa katika mikutano yake ya Kampeni ya kukiombea kura Chama Cha Mapinduzi (CCM), amekumbana na malalamiko kutoka kwa wanavikundi, waliosema kuwa kwenye vikundi vyao wanavyokopo wengine si waaminifu hivyo kuwaachia wenzao madeni.

"Jambo hili ni la msingi,kwani wanapounda vikundi vyao huwezi kuwapata wote wenye uwezo wa kufanya biashara, hivyo baadhi yao wanapoyumba kibiashara wanawaachia wengine madeni, nitakwenda kulisemea hili la mikopo binafsi," alisema Mkenge.

Aliongeza kuwa kuna akina mama wenye uwezo wa kumiliki biashara binafsi sanjali na akina baba wanaoweza kuzisimamia, kisha wao kuwapatia ajira wengine jambo litalosaidia kwa namna moja au nyingine kuongeza ajira katika maeneo mbalimbali.

"Ushauri wa mikopo binafsi nimeupokea nitakwenda kuufanyiakazi, dhamira ya Serikali kukopesha vikundi mikopo isiyo na riba inakabiliwa na changamoto katika bikundi, mchagueni Dkt. John Magufuli, mimi na Madiwani wote ili tukayasimame yote hayo" alisema Mkenge.

Kwa upande wake Meneja Kampeni wa mgombea huyo Yahya Msonde alizungunzia juhudi zilizofanywa na Rais Dkt. John Magufuli katika kipindi cha miaka mitano ikiwemo kuongeza idadi ya wanafunzi wa sekondari wapatao laki tano, na kufikia zaidi ya milioni moja.

"Tuwapogie kura za kutosha wagombwa wetu wote, lakini kwa Dkt. Magufuli ikibidi ziwe nyingi ili tulipe fadhira yetu kwake kwa kutupendelea wana-Bagamoyo kwani ametufanyia mambo mengi sana," alisema Msonde.

Alizungumzia kwa niaba ya wanawake wa Chasimba, mmoja wa akinaMama akijitambulisha kwa kina la Sada Farris alisema kuwa jambo hilo litakuwa msaada mkubwa kwao, kwani kuna changamoto kubwa katika urejeshaji wa mikopo kwa vikundi vingi.

Post a Comment

0 Comments