Na Faruku Ngonyani, Mtwara
Wito huo umtolewa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashasuri hiyo Bi Erica Yegella kwenye Mkutano wa Hadhara ulifanyika katika kijiji hiko cha Mkunwa.
Bi Yegella amesema kuwa kwa sasa ili wananchi waweze kujiongezeab kiuchumi na nimvyema wakachangamkia fursa ya kukopoa fedha hizo za Halmashauri , ambapo mpaka sasa bado kumekuwa na mwitikio mdogo haswa kwenye kundi la vijana.
Katika Mkutano hupo Wananchi wa kata ya Mkunwa wakifuatilia kwa makini Rai ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Mtwara Erica E. Yegella wakati wa mkutano wa hadhara uliolenga kuimarisha Uhusiano Kati ya Watumishi na wananchi Siku ya Tarehe 02 Oktoba, 2020.
Mkurugenzin huyo ameendelea kuwakumbusha na kuwasisitia wananchi hao kuendelea kufanya usafi wa mazingira yao ili kata hiyo iweze kuendana na hadhi ya Makao Makuu ya Halmashri hiyo.
Ikumbwe kwa sasa Halmashauri zote hapa nchini zinapaswa kutenga aslimia Kumi (10%) ya mapato yao ya ndani ili kutoa mikopo kwa Makundi ya Akina Mama (4% ),Vijana (4%) na Watu wenye ulimavu (2%).