Hukumu ya kifo yatekelezwa kwa wafungwa 13 Misri


Kituo cha televisheni cha kiraia kinachosadikika kuwa karibu na Chama cha Muslim Brotherhood nchini Misri, kimetangaza kutekelezwa kwa hukumu ya kifo kwa wafungwa.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook, kituo hicho kilichapisha majina ya wafungwa 13 waliokuwa wametiwa mbaroni kwa sababu za kisiasa na baadaye kuhukumiwa kifo nchini humo.

Taarifa hizo za utekelezwaji wa hukumu ya kifo kwa wafungwa 13 pia zilichapishwa na vituo vingine vya televisheni vinavyounga mkono upinzani, na kuendesha shughuli zao nje ya Misri.

Kituo kimoja  cha televisheni kilifikishia ndugu na jamaa wa karibu wa wafungwa 13 waliohukumiwa, na kuwataka waende katika hospitali ya Zinhum mjini Cairo endapo wangetaka kuchukuwa maiti zao.

Mamlaka husika ya Misri haikutoa taarifa zozote kuhusiana na tukio hilo.

Tangu mwaka 2013 baada ya mapinduzi ya kijeshi kutokea nchini Misri, watu wengi wamekuwa wakikamatwa kwa tuhuma mbalimbali na kuhukumiwa kifo.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Ujuwe Ugonjwa wa Busha

Kilimo cha Bamia