Mkuu wa IFM atoa wito wa msaada zaidi kwa mataifa ya Afrika


Mkuu wa shirika la fedha la kimataifa IMF Kristalina Georgieva amehimiza jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua zaidi kukabiliana na athari za kuanguka kwa uchumi kutokana na janga la virusi vya corona.

Akizungumza kwenye mkutano wa Afrika wa masuala ya uvumbuzi, Georgieva ameitolea wito benki ya dunia kuharakisha msaada wake wa kifedha kwa maataifa ya Afrika yaliyoathirika vibaya.

Wito wa kiongozi huyo umetolewa kuelekea vikao vya kila mwaka vya shirika la fedha duniani IMF na benki ya dunia na mwaka huu suala la kuzisaidia nchi zilizo kwenye mkwamo litakuwa kipaumbele.

Mkuu huyo wa IMF amesema taasisi anayoongoza itaendelea kuziombea msaada nchi za Afrika hususan kutoka taasisi za kimataifa na mataifa rafiki.

Benki ya dunia imeonya kuwa janga la virusi vya corona, kuanguka kwa bei za bidhaa na janga la nzige wa jangwani vimeathiri ustawi katika bara la Afrika na kuwaweka watu milinoi 43 kwenye hatari ya baa la njaa na umasikini uliopindukia.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items