Uingereza na Umoja wa Ulaya wasema mlango wa makubaliano ya kibiashara bado wazi

 


Uingereza na Umoja wa Ulaya wamesema leo mlango bado uwazi kwa makubaliano ya uhusiano wao wa baada ya Uingereza kujiondoa kutoka kwenye Umoja huo kufikiwa. 

Pande hizo mbili zimetaka kila mmoja kulegeza msimamo kwa ajili ya kunusuru mabilioni ya dola ya biashara kati yao. 

Huku ikiwa imesalia zaidi ya miezi miwili tu kabla Uingereza kumaliza kipindi cha makubaliano ya mpito yaliyokuwepo na Umoja wa Ulaya, mwafaka haujapatikana katika mazungumzo kuhusiana na makubaliano ya kibiashara huku ikiwa hakuna upande unaotaka kuwa wa kwanza kulegeza msimamo. 

Iwapo hakuna makubaliano yatakayopatikana, basi shughuli za viwanda, wafanyabiashara wa rejareja, wakulima na karibu kila sekta wataathirika. 

Haya yote yanakuja wakati ambapo uchumi wa nchi hiyo umeathirika vibaya na janga la virusi vya corona. Makamu wa Rais wa Umoja wa Ulaya Marcos Stefcovic amesisitiza kwa mara nyengine leo kuwa umoja huo bado unataka makubaliano ila si kwa thamani yoyote.


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia