Wafuasi wa upinzani wamekuwa wakipinga hatua ya rais ya kugombea kwa mara ya tatuImage caption: Wafuasi wa upinzani wamekuwa wakipinga hatua ya rais ya kugombea kwa mara ya tatu
Upinzani huko Ivory Coast umekataa mpango wa serikali wa kufanya mabadiliko katika tume ya uchaguzi kabla ya uchaguzi utakaofanyika wiki ijayo na kusisitiza kwamba utasusia uchaguzi huo.
Umoja wa Mataifa umeonesha wasiwasi wake kuhusu ghasia zinazoendelea ambazo zimesababisha vifo vya watu karibu saba huku zaidi ya 40 wakijeruhiwa, kwa mujibu wa serikali.
"Wagombea wa upinzani wanasisitiza kuwa wataendelea kuasi dhidi ya utekelezaji wa sheria na kusema wanataka taasisi za kimataifa kuingilia kati," Maurice Kakou Guikahue, msemaji wa upinzani, alizungumza na wanahabari Alhamisi.
Wagombea wawili wa upinzani – aliyekuwa rais, Henri Konan Bédié, na aliyekuwa waziri mkuu, Pascal Affi N'Guessan – walitangaza kususia uchaguzi mapema mwezi huu.
