Rais wa Urusi Vladimir Putin, amemwagia sifa Rais Recep Tayyip Erdoğan, na kusema kuwa miradi mingi kati ya Uturuki na Urusi imetekelezwa kwa uamuzi wa Rais huyo.
"Erdogan anafuata sera huru ya kigeni licha ya shinikizo." alisema Putin.
Vladimir Putin alijibu maswali kwenye mkutano wa Mazungumzo ya Kimataifa Valday, ambao alihudhuria kupitia njia ya video.
Wakizungumzia mvutano katika mashariki mwa Mediterania kati ya Uturuki na Ufaransa, Putin alijibu swali kuhusu upatanishi na kusema kuwa uhusiano mzuri kati ya Uturuki na Ufaransa unahitajika.
"Hata kama hatuna uhusiano mzuri sana na Ufaransa lakini tuna uhusiano endelevu. Tukizungumzia Uturuki. Uturuki ni jirani yetu. Nchi zote zote mbili ni muhimu katika uhusiano wetu.Sidhani kama kuna haja ya kuingilia ugomvi wa hao wawili. Nchi zinaweza kusuluhisha uhusiano wao wenyewe. Ingawa msimamo wa Erdoğan unaonekana kuwa mkali, najua yeye ni rahisi kubadilika. Inawezekana kuzungumza naye kwa lugha ya kawaida. Kwa hivyo natumai hali itaboreka. "
Akizungumzia uhusiano kati ya Uturuki na Urusi, Vladimir Putin amesema kuwa thamani ya biashara ya nchi mbili ni zaidi ya dola bilioni 20.
"Rais Recep Tayyip Erdoğan anafuata sera huru ya kigeni licha ya shinikizo. Tulifanya naye mradi wa TurkStream kwa muda mfupi sana. Lakini hatuwezi kufanya kwa haraka hivi na Ulaya."
Akikumbushia kuwa walikuwa na shida na Ulaya katika kutambua mradi wa bomba la gesi asilia la Mkondo wa 2, Vladimir Putin, amesema,
"Erdogan alisema, 'Tutafanya hiv,' na tukafanya hivyo. Uturuki, kwa ushirikiano wa kijeshi, iliamua kununua mfumo wa S-400 . Ni raha sana na salama kufanya kazi katika mazingira hayo. "
