Wagombea Wafunguka Makubwa Kwa Igp Sirro

 


Na Timothy Itembe Marwa.

wagombea wa vyama vya siasa mbalimbali Tarime/Rorya wamedai kuwepo uchaguzi wa huru na haki kwa msitakabali wa Katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.


Wakiongea mbele ya mkuu wa jeshi la polisi Tanzania(IGP),Saimon Sirro wakati kwenye kikao kilichowakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo wagombea ubunge kutoka Tarime na Rorya kilichokalia ukumbi wa bwalo la Bolisi walisema kuwepo uchaguzi huru na kaki.


Akiongea mgombea ubunge jimbo la Rorya kupitia Chama cha mapinduzi (CCM),Jafari Chege alisema kinachotakiwa sio wagombea kurushiana makombora na ubingwa wa kuongea badala yake wagombea wajali wapiga kura wao katika kudumisha Amani.


Chege alisema kuwa hakuna haja ya kuendelea kulaumiana na kutoleana matusi na kashifa mbali mbali za uchaguzi huku wapiga kura wanawatazana wanachokifanya kuwa hakiwaridhishi wapiga kura.


"Mimi nisema kuwa wagombea tukae chini natutafakari cha kwenda kuwaambia wapiga kura huku tukiuza sera za kuwa kama wananchi wakienda kutuchagua tutawafanyia nini badala ya kuendelea kurushiana makombora na lawama mbalimbali zisizokuwa na maana tubadilike"alisema Chege..


Mgombea huyo alitumia nafasi hiyo kumtaka IGP kuchukua hatua ya kukaa na wagombea wa Tarime Mjini na Vijijini kwa pande zote mbili CCM na CHADEMA kwasababu ya kuwasikiliza kwa kuwa  amegundua kuwa bado kuna shida kwa wagombea hao na kuwa akikaa nao atakwenda kugundua makubwa.


Naye Mgombea ubunge jimbo la Tarime mjini kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA),Esther Matiko alisema mbele ya mkuu wa polisi huyo kuwa ataenda kumshinda mgombea ubunge wa (CCM),Michael Kembaki kwa kura nyingi.


Matiko aliongeza kuwa jeshi la polisi lisitumike vibaya wakati likiwa kwenye majukumu ya kutekeleza kazi badala yake watende haki ya kikatiba kwa kila mgombea kwa sababu wote wanahaki sawa.


Matiko alitolea mfano vijana wake wa kampena kukamatwa na jeshi la polisi kwa madai ya kuwa wamehusika kufanya matukio mbalimbali ya ukiukwaji wa sheria huku wakipelekwa mahakamani ambapo  vijana wa CCM wakituhumiwa kufanya uhalifu wa matukio kama hayo wao hawakamatwi.


Mgombea ubunge viti maalumu kupitia CHADEMA,Tekra Johanes alitupia lawama jashi la polisi kutumika vibaya ambapo alisema kuwa kuna baadhi ya matukio wanatendewa wagombea wa CHADEMA lakini hatua hazichukuliwi.


Saimon Sirro ambaye ni mkuu wa jeshi la poliisi Tanzania(IGP), alisema lengo la kuitisha kikao hicho lilikuwa kuwakutanisha wagombea wa vya siasa Tarime na Rorya ili kuzungumza namna na kudumisha Amani.


Sirro aliongeza kuwa jeshi lake litaendelea kusimamia na kudumisha Amani hadi uchaguzi kwa mjibu wa sheria na atakaye shinda kwa kura nyingi ndiye atakaye enda kutangazwa sio vinginevyo.

Post a Comment

0 Comments