Wapinzani waliomba kiongozi anayetatua kero za wananchi-Sagini


Mbunge Mteule wa Jimbo la Butiama kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jumanne Sagini amesema kuwa awamu iliyopita wapinzani waliomba apatikane kiongozi atakayetumia muda mwingi kutatua kero za wananchi.

Akizungumza kwenye mkutano wa Kampeni uliofanyika mapema hii leo kijiji cha Bumangi Kata ya Muriaza kuwa Mungu alisikia kilio chao baada ya uchaguzi mkuu wananchi wakamchagua Rais John Magufuli ambaye alifanya mara mia ya walivyohitaji kwani ni kiongozi pekee aliyefaulu kudhibiti ufisadi na kuleta heshima serikalini.

"Ndugu zangu nawaombeni mumchague rais wetu Magufuli kwani toka aingie madarakani amekuwa humu nchini akifatilia utekelezaji na kero za wananchi na wala hajawahi kusafiri kwenda mataifa Ulaya," amesema Sagini.

Sagini ameeleza kuwa aliteuwa mabalozi ambao wanafatilia kwa umakini mambo ya kimaendeleo ikiwa ni pamoja na kutafuta wawekezaji na kushughulia mambo ya kiserikali katika nchi wanazoiwakilisha Tanzania.

Aidha amewaomba wananchi ifikapo Tarehe 28 Oktoba mwezi huu kuipigia kura CCM kuanzia nafasi za udiwani, ubunge na Rais kwa maendeleo ya Taifa

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items