Wizara ya mambo ya nje ya China imetoa wito kwa Marekani kuachana na mpango wa kuimarisha uhusiano wake na Taiwan, baada ya Washington na Taipei kutangaza kuwa watafanya mazungumzo ya kiuchumi mwezi huu.
Msemaji wa wizara hiyo Wang Wenbin ametoa kauli hiyo katika mkutano wa waandishi habari mjini Beijing.
China inaichukulia Taiwan ambayo inajitawala yenyewe kama jimbo lake lisilokuwa na haki ya kuwa na uhusiano rasmi na mataifa mengine.
