Ethiopia yadai kuwa mkuu wa WHO anaunga mkono TPLF

Mkuu wa jeshi la Ethiopia Jenerali Birhanu Jula amemshtumu mkuu wa Shirika la Afya Ulimwenguni - WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus, Muethiopia mwenzake, kwa kuzishawishi nchi jirani kupeleka silaha na msaada mwingine katika jimbo la Tigray, ambalo serikali kuu imekuwa ikipambana nalo kwa wiki mbili sasa. Jenerali Jula hakutoa ushahidi wowote wa madai yake.

 Amewaambia wanahabari kuwa Ghebreyesus aliwahimiza majirani ambao hawajatajwa "kupinga vita na kukipa silaha chama cha Ukombozi wa Watu wa Tigray - TPLF. 

Hakujatolewa kauli yoyote ya haraka kutoka makao makuu ya WHO wala kutoka kwa Tedros. Jeshi limesema vikosi vyake vinaukaribia mji mkuu wa Tigray, Mekelle. 

Serikali pia imesema inapanga kuwaerejesha wakimbizi waliokimbilia Sudan na kuwa inautuma ujumbe katika eneo hilo la kaskazini mwa nchi hili kutathmini hali ya kibinaadamu.
 

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi