Godbless Lema aachiwa huru na Polisi Kenya


Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema, ameachiliwa na polisi nchini Kenya baada ya kukamatwa kwa madai ya kuingia nchini humo kinyume na sheria.

Kwa mujibu wa wakili wake, George Wajackoyah, Lema ambaye alikua ameambatana na familia yake alikua akielekea jijini Nairobi kwa ajili ya kutafuta makazi ya muda baada ya kudai kutishiwa maisha.

Sasa mamlaka za kenya zimemruhusu Lema na familia yake kubaki nchini Kenya wakati akiendelea na taratibu za kuwa mhamiaji wa muda.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia