Idadi ya vifo kutokana na COVID-19 yakaribia kuvuka watu laki tatu barani Ulaya

 


Kwa mujibu wa hesabu za leo za shirika la habari la Reuters, Idadi ya watu waliokufa kutokana na maambukizi ya virusi vya corona, inakaribia kuvuka laki tatu barani Ulaya. 

Idara husika zinahofia, vifo na maambukizi vitaendelea kuongezeka katika majira ya baridi, licha ya matumaini ya chanjo inayotarajiwa kuanza kutumika mwaka ujao wa 2021. 

Ingawa idadi ya watu barani Ulaya ni asilimia 10 tu ya binadamu wote duniani, takriban robo ya maambukizi millioni 50.7 na vifo milioni 1.2 vimetokea katika bara hilo. 

Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, amesema leo kwamba jumuiya hiyo itatia saini kandarasi ya kuagiza dozi milioni 300 za chanjo dhidi ya COVID -19 baada ya kampuni za BioNtech ya Ujerumani na Pfizer ya Marekani kutangaza matumaini yaliyofikiwa katika hatua za mwisho za kutengeneza chanjo hiyo.


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items