Mjumbe wa Marekani asema itakuwa vigumu kurejea kwenye mkataba na Iran

 


Mjumbe wa Marekani anayeshughulikia suala la Iran amesema utawala wa Trump utaendeleza shinikizo dhidi ya Iran hadi siku rais mteule Joe Biden atakapoingia ikulu na anaamini kwamba itakuwa vigumu kwa utawala wa Biden kurejea kwenye mkataba wa nyuklia na Iran uliotiwa saini mwaka 2015. 

Mjumbe huyo Elliott Abrams alikuwa anazungumza na waandishi habari wakati wa ziara yake ya nchini Israel. 

Abrams amesema itajukulikana hapo baade iwapo Marekani itarejea kwenye mkataba huo. Hata hivyo rais mteuele Joe Biden amesema anatumai kuirudisha Marekani kwenye mkataba huo ambapo Iran ilikubali kuweka kikomo katika shughuli zake za kinyuklia. 

Kwa mujibu wa mjumbe wa Marekani Elliott Abrams, vikwazo vilivyowekwa na utawala wa Trump vitaendelea kutekelezwa hadi tarehe 20 mwezi Januari.


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items