Japan na Marekani zakubaliana kuhusu mkataba wa ulinzi

 


Waziri Mkuu wa Japan, Yoshihide Suga amesema Japan na Australia zimekubaliana kuhusu mkataba wa ulinzi kati ya nchi hizo mbili. 

Mkataba huo wa ushirikiano zaidi wa kiulinzi ni mfumo wa kisheria unaoruhusu majeshi yao kuzitembelea nchi za kila mmoja na kufanya mafunzo na operesheni za pamoja. 

Suga ameyazungumza hayo wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi habari na Waziri Mkuu wa Australia, Scott Morrison anayeizuru Tokyo. 

Nchi hizo mbili zimekuwa zikijadiliana kuhusu mpango wa ulinzi kwa miaka kadhaa ili kuimarisha uhusiano wao wa kiusalama, wakati ambapo China inaongeza ushawishi wake kwenye kanda hiyo. 

Hata hivyo, makubaliano hayo yanahitaji kuidhinishwa na wabunge.


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items