Mgaga Mkuu wa Serikali Prof.Abel Makubi leo amefanya ziara ya kikazi kwenye taasisi ya JKCI na MOI na kujionea hali ya utoaji huduma katika hospitali hizo.
Pof. Makubi amewashukuru na kuwapongeza Uongozi na watumishi wa taasisi hizo mbili kwa kazi kubwa wanazofanya katika kuwahudumia wananchi na kuwataka wafanye kazi kwa bidii na kwa uzalendo hususan kuwahudumia wananchi wasio na uwezo.
Vilevile amewataka kuendeleza mshikamano katika kuboresha huduma ili wananchi waweze kupata huduma nzuri na bora.
Kwa upande wa JKCI,Mganga Mkuu huyo aliwapongeza kwa kutumia mapato yao ya ndani kuboresha huduma kwenye hospitali hiyo.
Hata hivyo amewataka MOI kutoa wataalam wake kwenda kutoa huduma na ujuzi kwenye hospitali za kanda ili huduma za mifupa na mishipa ya fahamu isifuatwe Dar es Salaam pekee.



