Mpiga mbizi aliyewaokoa watu zaidi ya 100

Kwa miaka mingi, Shiva amekuwa akisadia polisi kupata miili ya watu katika ziwa Hussain Sagar kusini mwa India mji wa Hyderabad.


Siku moja alimuokoa mtu kabla ya kuruka majini na kunusuru maisha ya mtu kwa mara ya kwanza. Mwanahabari wa BBC wa Telugu Balla Satish amesema.


Shiva, ambaye anatumia jina moja anasema alikuwa na umri wa miaka 10 alipokutana na kundi la polisi ambao walijitolea kumlipa mtu yeyote ambaye angeweza kuopoa mwili karibu na kidimbwi.


Polisi nchini India wanalipwa pesa kidogo na mafunzo wanayopewa pia ni duni.


Wengi wao hawajui namna ya kuogelea na pia hawapewi pesa ya kutafuta wapiga mbizi wenye utaalamu.


Kwahiyo imekuwa kawaida wao kutegemea waogeleaji wasio na utaalamu.


Lakini Shiva alipojitolea, anasema, walishtuka. "Mwanzo, walikataa wakisema kwamba umri wangu ni mdogo sana. Lakini nikawashawishi hadi wakakubali," anakumbuka.


Alifanya kazi hiyo na kulipwa rupee 40, ambazo kwa sasa ni sawa na karibu dola 0.54 lakini wakati huo haikuwa pesa kidogo hivyo kwake.


Hiyo ilikuwa ni miaka 20 iliyopita.


Sasa hivi ana umri wa miaka 30 na bado anasaidia polisi wa eneo.


Shiva anaishi karibu sana na mto mkubwa unaofahamika kama Hussain Sugar.


Eneo hilo ni kivutio cha utalii na ziwa hilo pia linatumika wakati wa tamasha la Ganesha la kuzamisha masanamu majini ambayo Wahindi wanayachukulia kama miungu wao.


Lakini pia eneo hilohilo ni sehemu ambayo wengi hupoteza maisha yao na mara nyingi Shiva anasaidia polisi kuopoa miili ndani ya maji.


Wakati mwingine, pia huwasaidia kupata miili kutoka kwa mito na maziwa mingine katika mji.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia