Tume ya uchaguzi Myanmar kuanza kutangaza matokeo leo


Tume ya uchaguzi ya Myanmar inatarajiwa kutangaza matokeo ya awali ya uchaguzi hii leo. Hii ni baada ya raia kujitokeza kwa wingi jana kushiriki zoezi hilo licha ya kitisho cha virusi vya corona. 

Kiongozi wa nchi hiyo Aung San Suu Kyi anatarajiwa kushinda muhula mwengine mpya wa uongozi. Katika hesabu inayofanya kwenye ukurasa wake wa Facebook chama tawala nchini humo National League for Democracy NLD kinasema tayari kimeshashinda viti 15 kati ya 315 vinavyogombaniwa katika bunge la nchi hiyo ambalo lina wajumbe 425. 

Msemaji wa hicho chama tawala Myo Nyun ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa uchaguzi wenyewe ulikuwa wa amani. Jeshi ambalo liliitawala Myanmar kwa karibu miaka hamsini hadi kujiondoa kwake na kutoa nafasi kwa uongozi wa kiraia mwaka 2011, linachukua robo ya viti katika mabaraza yote ya bunge la nchi hiyo.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia