Mzozo wa viza za UAE kwa Pakistan


Pakistan imeomba serikali ya Falme za Kiarabu (UAE) kutatua suala la viza zilizotangazwa kusimamishwa wiki iliyopita.


Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistani Shah Mahmud Qurayshi, ambaye yuko katika mji mkuu wa Niamey nchini Niger kwa ajili ya Mkutano wa 47 wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC), alikutana na Waziri wa Serikali ya UAE Rim al-Hashimi.


Katika mkutano huo, Qurayshi alimweleza Hashimi juu ya shida wanazokumbana nazo raia kutokana na kizuizi cha viza za UAE kwa Wapakistani, na kusema kwamba tatizo hilo linapaswa kushughulikiwa haraka iwezekanavyo.


Mawaziri hao wawili pia walijadili uhusiano wa nchi mbili, janga la virusi vya corona (Covid-19) na hali ya masilahi ya pande zote.


UAE ilitangaza kusitisha utoaji viza kwa raia wa nchi 13 ikiwa ni pamoja na nchi 8 za Kiarabu kuanzia Novemba 18, hadi tangazo lingine litakapotolewa.


Wakati hakuna sababu yoyote iliyobainishwa kupelekea uamuzi huo kuchukuliwa, maelezo zaidi hayakutolewa kuhusu muda utakaodumu uamuzi huo na kumalizika.


Kuna zaidi ya raia milioni 1.5 wa Pakistan katika nchini ya UAE.

Post a Comment

0 Comments