Ndugai atoa neno kwa wabunge ambao hawajaapishwa


Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, amesema kuwa Rais Magufuli atalihutubia Bunge na Taifa siku ya Ijumaa ya Novemba 13, 2020, ikiwa ni ishara ya kuanza rasmi kwa shughuli za Bunge la 12.

Spika Ndugai ameyasema hayo leo Novemba 11, 2020, wakati akifungua shughuli za Bunge la 12 kikao cha 2, jijini Dodoma, ambapo shughuli zilizofanyika ni pamoja na kuapishwa kwa baadhi ya wabunge na kwa wale wenye udhuru zoezi la kuapa litafanyika siku za mbeleni.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items