Rais mpya wa Peru mwenye umri wa miaka 76 Francisco Sagasti ameapishwa hapo jana katika kikao maalumu cha bunge, ambalo lilipewa jukumu la kutatua mzozo wa kisiasa wa nchi hiyo ya Amerika ya Kusini.
Sagasti, kutoka chama cha mrengo wa kati cha Morado, atahudumu kama rais wa mpito hadi mwishoni mwa mwezi Julai mwakani, akikamilisha mamlaka ya Martin Vizcarra, ambaye kuondolewa kwake na bunge Jumatatu iliyopita kulichochea mgogoro huo.
Sagasti ameahidi kushughulikia janga la virusi vya corona kwa kupunguza kuenea kwa maambukizi bila ya kuathiri uchumi.
Mtangulizi wake wa karibu, spika wa bunge Manuel Merino, alilazimika kujiuzulu Jumapili, kufuatia siku kadha za maandamano.
