https://monetag.com/?ref_id=TTIb RC Byakanwa kushughulikia madai ya mishahara kwa wafanyakazi wa kampuni ya DOT Mkoani Mtwara | Muungwana BLOG

RC Byakanwa kushughulikia madai ya mishahara kwa wafanyakazi wa kampuni ya DOT Mkoani Mtwara

 



Na Faruku Ngonyani, Mtwara.

Serikali  Mkoa wa Mtwara imeahidi kushughulikia na kulitatua tatizo la kucheleweshwa kwa mishahara ya wafanyakazi wa kampuni ya DOT Inayojenga barabara ya Mtwara - Newala kwa kiwango cha Lami.

Kauli ya serikali inakuja baada ya wafanyakazi wa kampuni hiyo kugoma kuendelea na kazi kutokana na kucheleweshwa kwa malipo ya mishahara pamoja na michango ya mfuko wa hifadhi ya jamii.

Awali wakizungumza mbele ya mkuuu wa mkoa wa Mtwara Gelasius Gasper Byakanwa kwa niaba ya wafanyakazi wenzao Abdallah Simba pamoja na Hashimu Msuya wamesema wamefikia hatua ya kugoma baada ya uongozi wa kampuni hiyo kushindwa kuwalipa huku kukia hakuna taarifa yoyote.

Kwa upande wa afisa rasilimali watu wa kampuni ya DOT, MozaOZA JALO ameeleza kuwa kampuni yao imepatwa na ukata kutokana na kutolipwa fedha zao na serikali hali iliyopelekea TRA Kuzifunga akaunti za benki za kampuni hiyo kwa madai ya kodi na hivyo kushindwa kulipa gharama za uendeshaji wa Kampuni ikiwemo mishahara ya wafanyakazi.

Kufuatia maelezo hayo mku wa Mkoa wa Mtwara GELASIUS BYAKANWA amekiri kuwa na taarifa za kampuni hiyo kuidai serikali kiasi cha TSH; Billion 21 na hivyo kuwataka wafanyakazi hao kuwa watulivu wakati serikali  ikiendelea kulishughulikia suala hilo, na kwamba atahakikisha kufikia jumatatu ijayo wanalitatua.

Post a Comment

0 Comments