Samaki aina ya Jodari kupamba siku ya wavuvi Mkoani Mtwara


Na Faruku Ngonyani , Mtwara

Wavuvi Mkoani Mtwara wametakiwa kuhudhuri kwa wingi siku ya wavuvi hapa nchini ambapa kwa Mkoa wa Mtwara yanatarajia kufanyika tarehe 21 Novemba 2020 katika viwanja vya Feri vilivyopo Manispaa Mtwara Mikindani.

Hayo yamethibitishwa na Ndg Shabani Mayonzi ambaye ni mwenyeliti wa kamati ya maandalizi ambaye pia ni mwenyekiti wa Beach Management Unit (BMU) kutoka Msanga Mkuu.

Aidha Mayonzi amesema kuwa sherehe hizo za sikun ya  wavuvi zitazinduliwa tarehe 19 Novemba 2020 ambapo siku hiyo watachaguliwa wavuvi kumi (10) ambao watashiriki shindano la kumvua samaki aina ya Jodari na atakemvua jadari mwenye kg nyingi ndiye atakaeibuka kuwa mshindi.

Lakini  pia Mayonzi ametoa wito kwa wavuvi wote wa maji ya chumvi  na  baridi Mkoani Mtwara kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili waweze kutoa kero zao na ziweze kutatuliwa.

Kwa upande wa maandalizi afisa habari  na uhususiano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Isack Bilali amesema kuwa maandalizi yamekwishakamilika na sasa wanasuburi hiyo siku ili maadhimisho hayo yaweze kufanyika.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items